Home Yanga SC YANGA YATENGA MILIONI 180, WADAU WAOMBA KUIPA SAPOTI

YANGA YATENGA MILIONI 180, WADAU WAOMBA KUIPA SAPOTI


 TAARIFA kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinasema kwamba, kampuni moja kutoka nchini Uturuki, hivi karibuni ilifika klabuni hapo kwa ajili ya kufanya vipimo vya Uwanja wa Kaunda ili kuufanyia makadirio kabla ya kuanza ujenzi.


 Kwa muda mrefu, Yanga imekuwa katika mikakati ya kuukarabati uwanja huo ili uweze kutumika kwa mazoezi ya timu zao za vijana, wanawake na wakati mwingine ya wakubwa.

 Mtoa taarifa huyo alilidokeza kwamba: “Ni hivi karibuni tu, Waturuki walikuja kuangalia namna gani wanaweza kuukarabati Uwanja wa Kaunda ili uweze kutumika kama zamani.

 “Yanga inataka kuukarabati uwanja huu utumike kwa mazoezi na baadhi ya mechi za vijana na timu yetu ya wanawake, Yanga Princess ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.”

 Wakati Waturuki hao wakilenga zaidi kwenye uwanja, jumla ya shilingi milioni 180 zimetengwa kwa ajili ya kukarabati vyumba vya kulala kwenye Makao Makuu ya Klabu ya Yanga yaliyopo mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Dr Mshindo Msolla amesema kuwa wamedhamiria kuboresha vyumba ili kupunguza gharama za matumizi pamoja na kuwafanya wachezaji kuwa ndani ya kambi yao muda wote.

Msolla amewaomba wadau na wanachama wa Yanga wajitokeze kuweza kukarabati vyumba hivyo ili wawe sehemu ya historia ya mafanikio ya timu hiyo. 
SOMA NA HII  VIDEO: SERIKALI YATAJA KINACHOIPONZA YANGA KUSHINDWA KUPATA MATOKEO MAZURI