Home Simba SC BARBARA – HALI YA HEWA SUDAN SI KIKWAZO KWETU

BARBARA – HALI YA HEWA SUDAN SI KIKWAZO KWETU


UONGOZI wa klabu ya Simba, umesema hali ya hewa ya Sudan ni rafiki kwa vijana wao kupambana kupata matokeo katika mchezo wa makundi dhidi ya Al Merreikh.

Simba inakuwa mgeni katika mchezo huo wa Klabu Bingwa unaotarajiwa kupigwa Jumamosi kuanzia saa 1o jioni kwa saa badala ya ya ratiba ya awali iliyokuwa saa 4 usiku.

Simba inashuka dimbani kuwakabili miamba hao, ikiwa na hazina ya pointi sita kibindoni ambazo ilizivuna kutoka kwa AS Vita pamoja na Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Al Ahly.

Katika ukurasa wake wa Instagram Mtendaji Mkuu wa wanamsimbazi hao, Barbara Gonzalez amesema, kwa hali ya hewa iliyopo nchini humo haitawaathiri kwa chochote.

“Tumezoea kucheza mchana kwenye mechi zetu za Ligi Kuu na humidity ya hali ya unyevu Khartoum ni -12% na Dar es Salaam ni -70%,” amesema Barbara.

Simba imeondoka jana kuwafuata wapinzani hao katika mchezo huo, ikijidhatiti vilivyo kuanzia chakula mpaka sehemu ya kufikia wakifanya wao wenyewe kwa lengo la kujilinda.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO SIMBA SC WALIVYOFAULI NA KUFELI MECHI YA JANA DHIDI YA WYDAD....