Simba SC

SIMBA SC WAVUKA KIKWAZO KINGINE SUDANI

admin March 5, 2021 2:30 pm


SUDAN. KWA nyakati tofauti katika mashindano ya Kimataifa kama Ligi ya mabingwa Afrika na mengineyo kunakuwa na madai ya figisu inapofika kwenye vipimo vya covid 19.

Kikosi cha Simba kilifanya vipimo hivyo jana Machi 4 asubuhi katika kambi yao hapa katika hoteli ya nyota tano ya Al Salam.

Majibu ya vipimo hayo yametoka na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wote waliokuwa katika msafara majibu yao yametoka safi na hakuna mwenye maambukizi.

Kuwa safi kwa majibu hayo kazi inabaki kwa kocha wa Simba, Didier Gomes kuchagua wachezaji ambao anawataka kuwatumia katika mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba walivyoenda kucheza ugenini dhidi ya AS Vita hawakukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

BALAMA AREJEA DIMBANI YANGA, KUANZA MAZOEZI INJINIA HERSI AKIRI MAMBO MAGUMU YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply