BAADA ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kugawana pointi mojamoja na Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi, leo Machi 7 kinatarajia kutua ardhi ya Tanzania.
Tayari kikosi hicho kimeanza safari kutoka Sudan na leo kimewasili salama nchini Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kuibukia Dar.
Saa 4:30 asubuhi kinatarajia kuanza safari ya kurudi Tanzania ili kuendelea na maandalizi ya mechi zake zijazo.
Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zao zilizobaki ili kuweza kufikia malengo.
“Makosa kwenye mechi zetu ambazo zimepita tunayachukua na kuyafanyia kazi kwani kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi ndani ya uwanja,” .
Simba ikiwa inaongoza kundi A na pointi zake saba, mambo yanaonekana kuwa ni mazito kwa kuwa kwa sasa timu zote zina nafasi ya kusonga mbele na kutinga hatua ya robo fainali.
Al Ahly na AS Vita baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 wanafikisha jumla ya pointi nne huku Al Merrikh nayo inakuwa na pointi moja.
Hivyo ikiwa Simba itashindwa kupata matokeo kwenye mechi zake mbili nafasiya kuangukia nafasi ya tatu ni kubwa hivyo ni lazima ijipange ili kuweza kufikia malengo.