Uncategorized

ARGENTINA KUJADILI PICHA YA MARADONA KUTUMIKA KWENYE FEDHA YAO

admin December 10, 2020 10:47 am

 


SENETA Norma Durango wa Argentina amewasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo akipendekeza picha ya lejendari wa soka duniani, Diego Maradona, aliyefariki Novemba 25, 2020, iwekwe kwenye fedha za noti za nchi hiyo (Peso 1,000 sawa na Sh 27,600.)

 

Durango amesema lengo ni kumuenzi nyota huyo kwa heshima aliyolipa taifa hilo mwaka 1986 baada ya kuiwezesha Argentina kutwaa Kombe la Dunia na kuiandika historia ya nchi hiyo katika ramani ya soka duniani.

 

Noti hiyo itaonyesha sura ya Maradona huku upande mwingine ikionyesha goli maarufu alilofunga kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Uingereza 1986.

 

Maradona ambaye amewahi kuchezea vilabu vikubwa duniani ikiwemo Napoli ya Itali na FC Barcelona vilabu vingine kabla ya kustaafu soka kufuatia kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya, alifariki kwa tatizo la shambulio la moyo.

SIMBA YATOA TAMKO SAKATA LA KICHUYA BIASHARA UNITED KUBORESHA KIKOSI CHAKE DIRISHA DOGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply