Taifa Stars

STARS KUIFUATA KENYA LEO

admin March 13, 2021 5:47 am

 


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen leo Machi 13 kinatarajiwa kukwea pipa kuelekea Kenya ambapo kitakuwa na mechi mbili za kirafiki.

Mechi ya kwanza itakuwa Machi 15 na 18 ambapo ni maalumu kwa ajili ya kujenga hali ya kujiamini kwa kikosi hicho ambacho kimejumuisha nyota 40.

Maandalizi ya mechi hizo ni kwa ajili ya mechi za kufuzu Afcon ambapo itakuwa ni dhidi ya Equatorial Guinea ambayo itachezwa Machi 25 na dhidi ya Libya Machi 28 ambapo Stars ipo kundi J.

Poulsen amesema:”Maandalizi yapo sawa na nina amini kwamba kila mchezaji atapambana kusaka ushindi katika mechi ambazo tutacheza.

“Kila mmoja amekuwa akipambana kwenye mazoezi na inatoa picha kwamba tutafanya vizuri na tupo tayari katika kusaka ushindi,”.


MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI MRUNDI WA YANGA ATAJA WACHEZAJI WAKE ALIOWASAJILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply