Home Taifa Stars KIM KUIONGOZA STARS KWA MARA YA KWANZA LEO DHIDI YA KENYA

KIM KUIONGOZA STARS KWA MARA YA KWANZA LEO DHIDI YA KENYA


BAADA ya wiki tatu kupita tangu kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen  kupewa mikoba ya kukinoa kikosi hicho, leo saa 9:00 alasiri atakua na mechi ya kwanza dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’ kwenye uwanja wa Nyayo nchini Kenya.

Kim ambaye  amewahi kuifundisha timu hiyo kwa mwaka 2012 hadi 2014, alipata nafasi hiyo mwezi uliopita baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubalina kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Etienne Ndayiragije.

Kwa mujibu wa Kim mchezo huo wakirafiki atautumia kuwapa nafasi wachezaji wake tofauti kwa lengo la kuangalia kuwa yale wanayoelekeza mazoezini yanafanyika kwenye mechi.

“Tunatarajia kuwa na mchezo mzuri na wachezaji tofauti watacheza mechi hii ambayo lengo kuu zaidi ni kupata tathmini ya kikosi kizima kabla ya kwenda kwenye mechi za mbeleni hivyo hii itatusaidia kujua kua yale tunayofundisha yanatekelezeka kwa vitendo,” amesema Kim.

Baada ya mchezo huu wa leo, majirani hao wa Afrika Mashariki watajitupa uwanjani tena Machi 28 kucheza mchezo wa pili wa marudio mjini Nairobi yote hayo ikiwa ni maandalizi ya michezo yqa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2022).

Stars inatarajiwa kucheza na Guinea ya Ikweta Machi 25 ugenini kabla ya Machi 25 kupepetana na Libya kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Hata hivyo kwenye mchezo wa leo Stars itawakosa wachezaji wake baadhi wakiwemo wale wa Simba ambao wapo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji wengine watakao kosekana ni wale wanaocheza soka nje ya nchi na wanakabiliwa na majukumu mazito ya klabu zao licha ya kwamba baada ya mechi ya leo wataanza kuripoti kambini Kenya.

SOMA NA HII  TAA ZASIMAMISHA MECHI ZAIDI YA DK 16...TANZANIA VS UGANDA...ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI