Ligi Kuu

KOCHA MTIBWA SUGAR AWAPA KAZI WACHEZAJI WAKE

admin March 16, 2021 12:47 pm


 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wachezaji wake wana kazi ya kuongeza juhudi kwa ajili ya kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zijazo za mzunguko wa pili.

Mtibwa Sugari haijawa na mwendo mzuri ndani ya msimu wa 2020/21. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 24.

Mchezo wao wa mwisho wa ligi ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Thiery amesema kuwa wanatambua mwendo ambao wanakwenda nao sio mzuri jambo ambalo ni lazima lifanyiwe kazi.

“Ushindani umekuwa mkubwa hilo lipo wazi na matokeo ambayo yanapatikana bado yamekuwa ni mabaya kwetu.

“Tunachotakiwa kwa sasa ni kuona namna gani wachezaji wataweza kufanya vizuri wakati ujao uwanjani kwenye mechi zetu, bado tuna nafasi ya kurekebisha pale ambapo tulikosea,” amesema. 

SIMBA WATAMBA KUWAPIGA AL MERRIKH MAPEMA LEO KIKOSI CHA SIMBA RASMI KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA AL MERRIKH

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply