Azam FC

ISHU YA NAMUNGO KUONDOLEWA AZAM COMPLEX YATOLWEWA UFAFANUZI

admin March 17, 2021 4:47 pm


UONGOZI wa klabu ya Azam inayomiliki uwanja wa Azam Complex, ambao umekuwa ukitumiwa na Namungo kwa ajili ya michezo ya kimataifa umesema kuwa, bado unaendelea kufuatilia sababu za uwanja huo kuzuiwa kutumika kwenye michezo ya kimataifa wakati tayari ulikuwa na kibali.

Namungo imelazimika kucheza mchezo wake wa leo dhidi ya Pyramids ya Misri katika dimba la Mkapa, badala ya Azam Complex kutokana na zuio hilo.

Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam amesema: “Tunaendelea kufuatilia kama kuna mabadiliko yoyote ya vigezo vya uwanja unaopaswa kutumiwa kwa ajili ya michuano ya kimataiafa.

“Tunafanya hivi ili kuona kama kuna mapungufu yoyote basi turekebishe, maana tayari uwanja huu ulikuwa na ruhusa ya kutumika kwa michezo ya kimataifa,”

NYOTA WA YANGA KAMILI GADO KURUDI UWANJANI ORODHA YA WACHEZAJI 10 WA SIMBA WATAKAOIBUKIA KENYA, KESHO KAZI NYINGINE TENA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply