Yanga SC

MENEJA: METACHA NI MCHEZAJI WA YANGA

admin March 17, 2021 12:47 pm


 BAADA ya tetesi kueleza kuwa nyota wa Yanga, Metacha Mnata anatajwa kuingia anga za Simba, meneja wa mchezaji huyo amesema kuwa kipa huyo bado ni mali ya Yanga.

Mnata kipa namba moja ndani ya Yanga kwa sasa yupo nchini Kenya akiwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa kwa ajili ya mechi za kufuzu Afcon.

Habari zilikuwa zinaeleza kuwa mabosi wa Simba wamemalizana na Mnata ili akaongeze nguvu kwa mabingwa hao watetezi wanaoiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Mchezaji huyo, Jemedari Said amesema kuwa hakuna ukweli kuhusu suala hilo na Mnata ni bado mchezaji wa Yanga.

“Metacha Mnata ni mchezaji wa Yanga menye mkataba na kusema kwamba amesajiliwa na Simba wakati sio kweli ni kuikosea heshima klabu hiyo.

“Haitawezekana kwa Simba kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba. Kuna utaratibu wa usajili upo wazi kabisa na timu zote zinajua hivyo hakuna ukweli katika suala hilo,” .

LUNYAMILA: WAAMUZI MSITURUDISHE TULIKOTOKA HT: NAMUNGO 0-0 PYRAMIDS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply