Ligi Kuu

MTIBWA SUGAR YAMPASUA KICHWA HITIMANA THIERY

admin March 17, 2021 10:47 am


SAFU ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar inayoundwa na Kelvin Sabato inampasua kichwa kocha wao Hitimana Thiery kwa kuwa inashika rekodi ya kuwa safu namba moja kwa ubutu Bongo.

Kwenye Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ikiwa imecheza jumla ya mechi 22, imefunga mabao 9 na safu yake ya ulinzi imeokota jumla ya mabao 16.

Ikiwa ipo nafasi ya 14 na pointi zake 24 haijawa na mwendo mzuri jambo ambalo lilimfaya Zuber Katwila kubwaga manyanga na sasa yupo zake ndani ya Ihefu FC.

 Hitimana amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na watapambana kurejea kwenye hali yao ligi itakapoendelea.

“Ni kweli hatujawa kwenye mwendo mzuri, ila jambo la msingi ni kuweza kufanya maandalizi mazuri na kupambana kwa wakati ujao kupata kwa matokeo, ili upate matokeo ni lazima timu ifunge hilo lipo wazi tutalifanyia kazi,” amesema.

Safu ya Simba inaongoza kwa kufunga mabao mengi ikiwa imefunga jumla ya mabao 46 na imecheza mechi 20.

LUIS MIQUISSONE ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA MUDA WA NAMUNGO KUGANDAMIZIA KWA SIMBA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply