KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza ameanza mazoezi na kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi yakiwa ni maandalizi kuelekea mechi za kuwania kufuzu Afcon 2021 zitakazopigwa mwishoni mwa mwezi huu
Kurejea kwa nyota huyo ni ishara kuwa amepona majeraha yaliyomuweka nje tangu mwezi Januari mwaka huu
March 26 Burundi itakuja Tanzania kucheza mchezo wao dhidi ya Afrika ya Kati
Serikali ya Tanzania imeiruhusu Burundi kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo huo