Simba SC

UKUTA WA SIMBA WAKIMBIZA TATU BORA BONGO

admin March 17, 2021 12:47 pm


SAFU ya ulinzi ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imeweza kuweka rekodi ya kuwa ni namba moja kwa kuruhusu mabao machache.

Simba imefungwa mabao 9 ambayo ni machache kwa timu zilizo ndani ya tatu bora, ipo nafasi ya pili, Yanga ipo nafasi ya kwanza, ukuta wake unashika namba mbili kwa kuokota mabao mengi ambayo ni 14.

Ukuta wa Simba unaongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ambao wamekuwa na maelewano makubwa na ni chaguo la kwanza kwa Gomes.

Ukuta wa Yanga ulianza kuwa na maelewano mwanzo wa msimu ila kwa sasa taratibu uimara umeanza kumeguka chini ya Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.

ASUKILE: SIMBA WALITUNYIMA MABAO MENGI DHIDI YA JKT LUNYAMILA: WAAMUZI MSITURUDISHE TULIKOTOKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply