Ligi Kuu

HITIMANA: KAZI BADO INAENDELEA

admin March 19, 2021 12:47 pm


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa timu yake haijavunja kambi inaendelea na maandalizi ya mechi zake za ligi.

Kwa sasa ligi imesimama kwa muda kwa ajili ya maandalizi ya timu za taifa kuweza kucheza mechi za kufuzu Afcon ambapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ipo Kenya.

Mtibwa haijawa kwenye mwendo mzuri msimu huu ikiwa imecheza jumla ya mechi 22, ipo nafasi ya 14 imekusanya pointi 24.

Hitimana ameliambia Spoti Xtra kuwa wachezaji wameendelea kuwa kwenye maandalizi ya mechi zao ili waweze kurudi kwa kasi.

“Hatujavunja kambi tunaendelea na mazoezi ili kuwa imara kwa ajili ya mechi zetu zijazo, ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi pia tunapambana kupata matokeo chanya.

“Tumekuwa tukipata matokeo ambayo si rafiki kwetu kwenye mechi zetu hilo lipo wazi hivyo ambacho tunafanya kwa sasa ni kupambana kurudi kwenye ubora,” .

ZIMBWE JR AWEKA REKODI YAKE LIGI YA MABINGWA AFRIKA JOSE MOURINHO MAMBO MAGUMU SPURS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply