Home Simba SC MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF

MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF

WINGA wa klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morroco, Saimon Msuva amesema kuwa anatamani kukutana  na klabu ya Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani anaamini itakuwa mechi nzuri sana katika msimu huu wa ligi hiyo.

Saimon Msuva katika msimu huu wa ligi hiyo akiwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao miwili katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia michuano hiyo Msuva amesema: โ€œNatamani kuona tunakutana na Simba katika hatua ya robo fainali kwani utakuwa mchezo mzuri sana katika ligi ya mabingwa msimu huu kwani itazikutanisha timu bora ambazo zote zinafanya vizuri kwa sasa.

SOMA NA HII  SIMBA YAWASHUSHIA AL AHLY BEI YA KUMPATA LUIS..SASA WANATAKA 650K TU