Simba SC

MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF

admin March 19, 2021 4:47 pm

WINGA wa klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morroco, Saimon Msuva amesema kuwa anatamani kukutana  na klabu ya Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani anaamini itakuwa mechi nzuri sana katika msimu huu wa ligi hiyo.

Saimon Msuva katika msimu huu wa ligi hiyo akiwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao miwili katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia michuano hiyo Msuva amesema: “Natamani kuona tunakutana na Simba katika hatua ya robo fainali kwani utakuwa mchezo mzuri sana katika ligi ya mabingwa msimu huu kwani itazikutanisha timu bora ambazo zote zinafanya vizuri kwa sasa.

SAIDO AREJEA RASMI KAZINI PLUIJM ANA JAMBO NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply