news

FIFA YAMLILIA RAIS MAGUFULI

admin March 20, 2021 6:47 am


 JUMUIYA ya soka kimataifa ‘FIFA’ limetuma salamu za rambirambi kwa shirikisho la soka nchini TFF kufuatia kifo cha Rais, Hayati, Dk.John Pombe Magufuli kilichoripotiwa kutokea siku ya Jumanne, 17 Machi 2021 kwenye Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo.


 Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, Rais wa jumuiya hiyo Gianni Infatino ameandika kuwa:-“Ilikuwa hisia ya huzuni kupata taarifa za kifo cha Rais Dk.John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

 

 “Tunapenda kuungana na wote wanaotoa salam za pole kutoka pande zote Duniani. Akiongoza toka mwaka 2015, kiongozi mwenye haiba ya juu, aliyetambulika kwa maono yake, uzalendo, matendo ya Utawala bora na kupiga vita rushwa na umasikini, Rais, Dk.John Pombe Magufuli hatosahaulika.

 

“Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, tunapenda kutoa pole kwa shrikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’, Serikali na watanzania kwenye kipindi hiki kigumu”.


MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI GOMES :- SIMBA BADO SANA KWA UBINGWA WA AFRICA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply