IMERIPOTIWA kuwa uongozi wa Klabu ya Al Merrikh ya Sudan umetinga Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuripoti kuhusu suala ambalo wameliita ni kuhujumiwa na Klabu ya Simba ya Tanzania kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwenye mchezo wa marudio uliochezwa Machi 16, Uwanja wa Mkapa na Simba kushinda mabao 3-0, Klabu ya Al Merrikh iliweka wazi kuwa wachezaji wake 8 waliripotiwa kwamba wana Corona muda mfupi kabla ya mechi jambo ambalo walidai kwamba ni hujuma.
Miongoni mwa wachezaji ambao wametajwa kuwa na Corona ni Abdul Rahman Karngou, Altaj Yaqoub, Bhakit Khamis, Ramadan Ajab, Tony, Bakir Al Madina, Saif Al-Damazin, Emad Abdul-Manim.
Al Merrikh wametinga ofisi za Caf na kupeleka majibu yao ambayo wanadai kwamba yalikuwa yaanaonyesha kwamba hakuna mchezaji mwenye Corona bali ilikuwa ni ujanja wa Simba kutaka kuihujumu timu hiyo.