Ligi Kuu

MAGUIRE AAMBIWA KUMKABA FULLY ZULLY MAGANGA WA RUVU NI DHARAU

admin March 22, 2021 4:47 am


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa kwa mshambuliaji wao matata Fully Zully Maganga kukabwa na beki wa Klabu ya Manchester United, Harry Maguire itakuwa dharau kubwa.

Maneno hayo yamewekwa wazi ikiwa ni muda mfupi baada ya Klabu ya Manchester United kupoteana kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Leicester City.

United ikiwa na beki wake ghali, Maguire ilikubali kichapo cha maba 3-1 jambo ambalo limewaondoa kwenye reli United na harakati za kutimiza lengo la kutwaa taji la FA.

Kupitia ukurasa wao wa Twiter, Ruvu Shooting waliadika namna hii:”Fully Zullu Maganga akabwe na Mwagwaya, (Maguire) kweli si dharau hizi,”.

Maguire mwenyewe amesema:”Tulikuwa tunahitaji ushindi ila tumekosa hakuna wa kumlaumu kwa wakati huu na hakuna namna ya kufanya zaidi ya kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.

Ilikuwa ni Uwanja wa King Power mchezo wa robo fainali Kombe la FA.

MBELGIJI WA SIMBA AMLILIA MAGUFULI YANGA: TUNAAMINI YALIYOFANYWA NA MAGUFULI YATAENDELEA KUTENDEKA ILI KUMUENZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply