Simba SC

ERASTO NYONI KUWAJIBU NAMNA HII WALE WANAOMUITA MZEE

admin March 24, 2021 1:47 pm


ERASTO Nyoni, kiraka wa kikosi cha Simba amesema kuwa wale ambao wanasema kwamba amezeeka atawajibu kwa vitendo uwanjani.

Mkongwe huyo kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambacho kesho kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Equatorial Guinea mchezo wa kufuzu Afcon.
Mashabiki wengi wamekuwa wakimlalamikia juu ya uwezo wake wakidai kuwa ni mzee anapaswa kutundika daluga jambo ambalo nyota huyo amelipuuzia na kuliweka kando.
Nyoni amesema:”Najua wapo ambao wanasema kwamba mimi ni mzee hao siwezi kuwazuia kwa kuwa ni haki yao kuongea.

“Ila kwangu mimi naona kwamba nitawajibu kwa vitendo uwanjani watajua kwamba mimi ni mtu wa aina gani kila kitu kitakuwa wazi kwani mpira ni mchezo wa wazi,” amesema.
NYOTA WAWILI WA AZAM FC KAZINI NA TIMU YAO YA TAIFA YA UGANDA KOCHA SIMBA: TUTAWAFUNGA VITA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply