Azam FC

NIYONZIMA WA AZAM FC KUWEKWA KANDO MSIMU UJAO

admin March 26, 2021 6:47 am


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Azam FC, Ally Niyonzima huenda atawekwa kando msimu ujao kutokana na kushindwa kufiti mipango ya mabosi hao wa Dar.

Niyonzima ambaye ni ingizo jipyakutoka Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha kubwa.

Habari zimeeleza kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC amewaomba mabosi wa timu hiyo kumtafuta kiungo mwingine jambo ambalo linaashiria kuwa safari ya kiungo huyo imefika tamati.

“Kocha anahitaji kupata kiungo mkabaji mwingine kwani bado huyu ambaye yupo bado hajaweza kufiti hivyo atakayesajiliwa atakuwa katika ubora,” ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit alisema kuwa kuhusu usajili wa timu hiyo wanachotazama ni ripoti ya ya kocha.

KMC YAUNGANA NA WATANZANIA KUMLILIA MAGUFULI, YASITISHA MIPANGO KAZI WAPINZANI WA SIMBA AS VITA KUJA BONGO MAPEMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply