Simba SC

WAPINZANI WA SIMBA AS VITA KUJA BONGO MAPEMA

admin March 26, 2021 6:47 am


 KOCHA Msaidizi wa Klabu ya AS Vita ya DR Congo, Raoul Shungu amesema kuwa watawahi mapema kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

AS Vita inatarajiwa kumenyana na Simba Aprili 3, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo wa kwanza walipokutana Congo, Simba ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Simba kusepa na pointi tatu mazima.

Ikiwa Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye kundi A na pointi zake 10 inatarajiwa kumenyana na AS Vita iliyo nafasi ya tatu na pointi zake nne.

Kocha huyo amesema:”Mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa na ushindani mkubwa hivyo ili tupate matokeo chanya ni lazima tuwahi kufika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho.

“Wachezaji wetu wanatambua kwamba haitakuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kwamba Simba imekuwa ikipata matokeo chanya kwenye mechi zake inazocheza nyumbani,” amesema.

NIYONZIMA WA AZAM FC KUWEKWA KANDO MSIMU UJAO CLATOUS CHAMA APEWA JUKUMU ZITO MBELE YA AS VITA, LIGI YA MABINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply