Home Simba SC KIPA NAMBA MOJA WA SIMBA MANULA AFUATWA NA WAARABU

KIPA NAMBA MOJA WA SIMBA MANULA AFUATWA NA WAARABU

 


WAKATI kipa wa Simba, Aishi Manula akiendelea kung’ara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Rais wa Klabu ya Al-Merrikh SC ya Sudan, Adam Sudacal yupo tayari kutoa ofa ya zaidi ya Sh milioni 230 ili amweze kuinasa saini ya kipa huyo.


Manula bado yupo kwenye mkataba na Klabu ya Simba anaonekana kusakwa na miamba hiyo ya Sudan, baada ya kutengeneza rekodi ya kutofungwa bao lolote katika michezo ya Kundi A kati ya minne ambayo timu yake imecheza.

 

Awali mchezo wake wa kwanza katika hatua hiyo kusimama langoni ni dhidi ya AS Vita wakiwa ugenini wakashinda bao 1-0, wa pili ni dhidi ya Al Ahly ya Misri uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Darambapo Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Luis Miquissone.

 

Mchezo wa tatu dhidi ya Al-Merrikh wakiwa ugenini hakucheza kwa kuwa hakuwa fiti kiafya na nafasi yake ikachukuliwa na Beno Kakolanya, matokeo yakiwa 0-0


Manula alisimama langoni katika mchezo wa nne dhidi ya Al-Merrikh akiokoa michomo kadhaa ambayo wapinzani walipata nafasi za wazi kwenye Uwanja wa Mkapa, Simba ikishinda kwa mabao 3-0.


Habari zinaeleza kuwa inaonekana harakati za Kocha Mkuu wa Al-Merrikh ya Sudan, Lee Clark anaitaka zaidi saini ya Manula ili aendelee kukiboresha kikosi hicho jambo ambalo linadaiwa kuwafanya miamba hiyo kuzidi kupambana kumpata kipa huyo.

 

“Naomba nikwambie tu kuwa ni kweli nilisikia Manula kama anauliziwa na Waarabu flani hivi, ila kwa kuwa sikuwa na wazo lolote juu ya kutakiwa na jamaa hao kiukweli sikufatilia alichokuwa anatafutiwa.

 

“Isipokuwa nakumbuka nilikutana na mmoja wa wachezaji hapa, akaniambia naona dili la Aishi kwa Wasudan linaelekea ukingoni, nilipomuuliza kwa nini ndiyo akaniambia kuwa kuna jamaa kutoka Sudan walienda kumuona kwenye mechi ya Stars na Equatorial Guinea,” kilisema chanzo hicho.

 

Hivi karibuni kulikuwa na hizo taarifa kuwa Al-Merrikh imekuwa na mpango huo wa kumuwania Manula jambo ambalo muda wowote endapo Simba kupitia kwa mwekezaji wao, Mohamed Dewji ‘Mo’ watakubaliana nao juu ya ofa yao waliyotoa wakimtaka aende kujiunga na kikosi chao, inaweza kuwa dili zuri.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA TETESI ZA KUACHWA ZIMEZIDI...GADIEL MICHAEL AFANYA JAMBO SIMBA..OKRAH NAYE AZIDI KUNG'ARA....

 

Lakini kwa upepo ulivyo, halitakuwa jambo jepesi kwa Simba kumruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa kuwa wamekuwa wakiimarisha usajili wao ili kuwa bora katika ngazi ya kimataifa.