KIONGOZI wa zamani wa benchi la ufundi la Klabu ya Watford, Filippo Giraldi ameweka wazi kwamba mabosi wa Manchester United walikuwa wanahitaji saini ya kiungo wao Ismaila Sarr, msimu uliopita.
United ilikuwa imeweka nguvu kubwa kwenye kusaka saini ya kiungo wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ila dau lake la pauni milioni 100 liliwafanya mabosi wa timu hiyo wasitishe suala la kukamilisha dili hilo.
Baada ya kuona kwamba wamekwama kumpata Sancho waliongeza nguvu kwa Sarr wa Watford ili wapate saini ya winga huyo ambapo dau lake lilitajwa kuwa pauni milioni 40.
Giraldi amesema kuwa alikuwa miongoni mwa viongozi ambao walizungumza na United kuhusu dili hilo la nyota huyo kutua ndani ya kikosi cha United kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.
“Tulikuwe kwenye mazungumzo ya karibu na United kuhusu Sarr nami nilikuwa kwenye mazungumzo hayo ila tulishindwa kufikia makubaliano, nadhani labda inatokana na Sarr kuwa mdogo.
“Nadhani alikosa fursa hiyo ya kujiunga na United ila aliweza kufanya vizuri alivyobaki ndani ya Watford na ana uwezo mzuri ambao unazidi kukua kila iitwapo leo,” .