Taifa Stars

STARS WATAJA SABABU YA KUPOTEZA MCHEZO MBELE YA EQUATORIAL GUINEA

admin March 28, 2021 12:47 pm

 


SELEMAN Matola, Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars amesema kuwa walishindwa kupata matokeo mazuri mbele ya Equatorial Guinea baada ya kushindwa kutumia nafasi walizopata.


Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea Machi 25 na leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Libya, Uwanja wa Mkapa.


Kupoteza mbele ya Equatorial Guinea kumeyeyusha matumaini ya Stars kufuzu Afcon, nchini Cameroon hivyo leo wanacheza na Libya ambayo nayo haijafuzu Afcon.


Matola amesema:” Tunajua kwamba Watanzania wanapenda kuona timu inapata matokeo mazuri ila tulishindwa baada ya kushindwa kutumia nafasi chache ambazo tulipata.


“Makosa tumeyafanyia kazi tunaamini leo tutapambana kupata ushindi mbele ya Libya hivyo dua muhimu kwani wachezaji wapo tayari,” .

STRAIKA MNYARWANDA AZITAMANI SIMBA, YANGA OLE GUNNAR KUPEWA MKATABA MPYA KUINOA TIMU HIYO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply