Home Simba SC HATMA YA KAHATA NDANI YA SIMBA MSIMU UJAO IKO HIVI..!!

HATMA YA KAHATA NDANI YA SIMBA MSIMU UJAO IKO HIVI..!!


UWEZO wa nyota wa Simba, Francis Kahata ndio tiketi yake itakayomnusuru kuachwa na wekundu  wa Msimbazi Simba kuelekea usajili wa msimu ujao 2021/22.

Hivi karibuni ilitokea sintofahamu baada ya uongozi wa Simba kumpeleka nyota huyo kwa ajili ya michuano ya Kimataifa pekee na kumuondoa katika ligi kuu.

Baada ya mabadiliko hayo gazeti la Mwanaspoti lilifanya mahojiano na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ aliyekubali nyota huyo kupelekwa katika michuano ya kimataifa ili aweze kupata nafasi kwa kuwa ana uzoefu mkubwa huko tofauti na Ligi ushindani ulikuwa mkubwa uliomfanya kukosa nafasi.

“Kahata ni kweli tumempeleka kwenye michuano ya Kimataifa ili apate nafasi ya kucheza na mkataba wake unakaribia kumalizika, lakini kocha wetu akimuhitaji kuendelea kuwepo sisi hatuna shida tunamwongezea tu,”alisema Try Again.

Baada ya kauli hiyo ya uongozi, Gazeti la Mwanaspoti lilimtafuta Kocha Mkuu Didier Gomes kujua hatima ya nyoa huyo na kusema, mpaka sasa hana mchezaji atakayemwacha bali ni kila mmoja kuhakikisha anaonyesha uwezo wake binafsi ambao utamshawishi ili aweze kubaki.

“Siwezi kuzungumza sasa kuwa ni mchezaji gani namuacha, Simba kila mchezaji ni mzuri na wote nimewakuta, uwezo na jitihada za mchezaji yoyote yule ndizo zitambakiza Simba, kwa sasa niko bize na kombe la ligi, FA na michuano ya Kimataifa siwezi kuwachanganya wachezaji wangu,” alisema Gomes.

Credit- Mwanaspoti

SOMA NA HII  KISA USHINDI WA JANA...MANARA AIPONGEZA NA KUINANGA SIMBA..."KULA NYAMA YA MTU KUNANOGA..."...