Home Yanga SC BAKARI MWAMNYETO KUWEKWA KANDO YANGA, HUYU HAPA KUCHUKUA MIKOBA YAKE

BAKARI MWAMNYETO KUWEKWA KANDO YANGA, HUYU HAPA KUCHUKUA MIKOBA YAKE


 BAKARI Mwanyeto anatajwa kuwekwa kando kwa muda ndani ya kikosi cha Yanga ili kumpisha nyota mpya Dikson Job kwenye upande wa safu ya ulinzi.

Mwamnyeto amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano na mshikaji wake Lamine Moro kwenye kulinda ngome ya Yanga ila wamekuwa wakifanya makosa ambayo yanaigharimu timu hiyo.

Kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa wakati wakiokota jumla ya mabao matatu unafanya iwe rekodi yao ya kwanza msimu huu kuokota mabao mengi nyavuni kwenye mchezo mmoja.

Pia walikwama kuweka umakini wakati walipokutana na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Machi 4.

Baada ya dakika 90, ubao wa pale Mkwakwani ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga jambo lililofanya timu hiyo inayonolewa na Cedric Kaze kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa tayari Job ambaye ni ingizo jipya kutoka ndani ya Mtibwa Sugar ameanza kufanya mazoezi mepesi na atakabidhiwa majukumu ya Mwamnyeto.

“Kijana Job yupo tayari kuanza kucheza mechi za ushindani kwa kuwa majeruhi aliyokuwa anasumbuliwa nayo yamepona na ameanza mazoezi mepesi.

“Ana jukumu la kubeba mikoba ya Mwamnyeto kwa muda ili kuweza kumpa nafasi ya kupumzika kwa kuwa hajawa sawa kisaikolojia baada ya kupata matatizo ya kifamilia, ” ilieleza taarifa hiyo.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kupoteza kwao kunatokana na makosa ambayo wanayafanya uwanjani hivyo watayafanyia kazi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO....UNAAMBIWA NABI HUKO YANGA HATAKI MZAHA...APANIA KUUA 'SISIMIZI KWA RUNGU'....