Home Taifa Stars BEACH SOCCER YARAHISISHIWA KAZI KUFUZU AFCON

BEACH SOCCER YARAHISISHIWA KAZI KUFUZU AFCON


 BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa kuchezwa mechi zote mbili Dar za kufuzu AFCON kumewarahishia kazi kufikia malengo.

Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni inatarajiwa kumenyana na timu ya Taifa ya Burundi, Machi 30 na Aprili 3 ambayo yote itachezwa Dar.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pawasa alisema kuwa kitendo cha Burundi kuomba mechi yao pia ichezwe Dar kumewarahisishia kazi ya kupata matokeo chanya.

“Maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa kwa kuwa wachezaji wanaonyesha morali kubwa, kuchezwa kwa mechi zote Dar kumetupunguzia ile presha ya kucheza ugenini hivyo mechi zote itakuwa ni jukumu letu kushinda na inawezekana,” alisema Pawasa.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO BILIONI 17 ZILIVYOYEYUKA KWA TAIFA STARS...MCHONGO MZIMA HUU HAPA...