Home Habari za michezo HIVI NDIVYO BILIONI 17 ZILIVYOYEYUKA KWA TAIFA STARS…MCHONGO MZIMA HUU HAPA…

HIVI NDIVYO BILIONI 17 ZILIVYOYEYUKA KWA TAIFA STARS…MCHONGO MZIMA HUU HAPA…

Habari za Michezo leo

Bingwa wa michuano ya Afcon 2023 Ivory Coast amejinyakulia kitita cha dola milioni 7 (7,000,000) ambayo ni zaidi ya Bilioni 17.7 kwa fedha za Kitanzania baada ya kuifunga Nigeria magoli 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Februari 11-2024 mjini Abdijan nchini Ivory Coast.

Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na nyota Frank Kessie na Sebastian Haller huku bao la Nigeria likifungwa na mlinzi Troost Ekong huku Super Eagles ambao ni washindi wa pili wameondoka na Dola Milioni 4 (4,000,000) zaidi ya Bilioni 10.1 kwa fedha za Kitanzania.

Upande mwingine, Golikipa Ronwen Williams wa Afrika Kusini ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano,Emilio Nsue Lopez ameshinda tuzo ya mfungaji bora baada ya kuifungia Equatorial Guinea mabao5 ilhali nahodha wa Nigeria William Troost-Ekong akichaguliwa kuwa mchezaji bora mashindano ya Afcon 2023.

Inafahamika kuwa Tanzania ilishiriki mashindano ya AFCON kwa mara ya tatu ambapo tuliambulia alama 2 mara baada ya kutoka sare na Congo na Zambia katika michezo ya kundi F.

Kabla ya kwenda Ivory Coast, Serikali iliitisha harambee kwa ajili ya kuchangia timu za taifa katika kuzipa hamasa kwenye mashindano mbalimbali.

SOMA NA HII  BACCA AFICHUA YANAYOENDELEA YANGA..."SIWEZI KUTAJA SIFA ZA MCHEZAJI...AFUNGUKA HAYA