Home Azam FC KATWILA AKWAMA MBELE YA AZAM FC

KATWILA AKWAMA MBELE YA AZAM FC

 


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya mipango yake ya kusepa na pointi sita mbele ya Azam FC msimu wa 2020/21 imekwama kwa kufungwa nje ndani.


Mchezo wa kwanza walipokutaba Mbeya, Ihefu ilikubali kichapo cha mabao 2-0 ambapo watupiaji walikuwa ni Ayoub Lyanga na Idd Seleman. 


Huo ulikuwa ni mchezo wa Kwanza mwa Katwila baada ya kujiunga na Ihefu akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar  na jana Machi 11 ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.


Mabao yalifungwa na Idd Seleman ambaye alitupia mawili na Lyanga naye alitupia bao moja hivyo Ihefu imefungwa jumla ya mabao matano na kuacha pointi sita mikononi mwa Azam FC. 


Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya tatu na Ihefu FC ipo nafasi ya 16 na pointi zake ni 20.

SOMA NA HII  AZAM FC KAMILI KUWAAVAA WAARABU WA MISRI