Home news KMC YAUNGANA NA WATANZANIA KUMLILIA MAGUFULI, YASITISHA MIPANGO KAZI

KMC YAUNGANA NA WATANZANIA KUMLILIA MAGUFULI, YASITISHA MIPANGO KAZI


 UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa kwa sasa umesitisha mipango kazi yote kuhusu mazoezi kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, John Pombe Magufuli.

Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 kutokana na matatizo ya moyo kwa mujibu wa Samia Suluhu ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais ila kwa sasa ni Rais kwa mujibu wa katiba.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa timu hiyo haijavunja kambi bali ilitoa mapumziko ambayo muda wake umekwisha na sasa wachezaji wamerejea kambini.

“Kambi hatujavunja kwa kuwa tuliwapa wachezaji wetu mapumziko ya muda nane ambapo yalipokamilika walirejea kambini Machi 20, baada ya taarifa ya msiba tukasitisha program zote.

“Baada ya taratibu za msiba kukamilika nina amini kwamba tutatoa taarifa kwa mashabiki na Watanzania ili kujua nini kinaendelea ndani ya KMC ila kwa sasa tunaungana na Watanzania kuomboleza kuondokewa kwa kiongozi wetu,” amesema.

Leo Machi 26, mwili wa Magufuli unatarajiwa kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Chato.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUPATA NAFASI YANGA..'SURE BOY' YAMKUTA YA KUMKUTA...KILAANI KUPOTEZA TENA NAFASI...