Home Simba SC MAKIPA WAWILI WA SIMBA WAWEKA REKODI YAO CAF

MAKIPA WAWILI WA SIMBA WAWEKA REKODI YAO CAF

[the_ad id="25893"]


 KIPA namba moja wa Klabu ya Simba, Aishi Manula ameweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika bila kufungwa hatua ya makundi.

Wakati Manua ambaye ni kipa namba moja akiweka rekodi ya kukaa langoni bila kufungwa na kipa namba mbili naye Beno Kakolanya naye amekaa langoni mechi moja bila kupoteza.

Makipa wawili wa Simba wameweza kuweka rekodi kwenye hatua ya makundi kwa kucheza mechi nne bila kufungwa ambazo ni dakika 360 bila kuokota mpira wavuni.

Manula amekaa langoni kwenye mechi tatu ambazo ni dakika 270 ilikuwa AS Vita 0-1 Simba, Simba 1-0 Al Ahly 0 na Simba 3-0 Al Merrikh.

Kakolanya kipa namba mbili yeye kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo yanasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) amekaa kwenye mechi moja ilikuwa Al Merrikh 0-0 Simba.

SOMA NA HII  SIMBA WALIVYOITUNGUA RUVU SHOOTING KWA STAILI YA 'KI.REAL MADRID'...SASA NI KAZI KAZI MPAKA ....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here