Home Yanga SC MAKOCHA 72 WAOMBA KAZI YANGA

MAKOCHA 72 WAOMBA KAZI YANGA

 


WAKATI kwa sasa kikosi cha Yanga kinachoongoza Ligi Kuu Bara kikiwa na pointi 50 kikiwa chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi, UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuna maombi ya makocha zaidi ya 73 ambao wameomba kukinoa kikosi hicho. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mchakato wa kumtafuta Kocha mpya unaendelea na atakuja mapema kabla mzunguko wa pili haujakamilika. 

“Tumefanya mabadiliko Kwenye benchi la ufundi kama ambavyo watu wameskia kwa kuwa timu ilikuwa haipati matokeo . Mambo haya yameamuliwa na uongozi.


“Mwalimu mwenyewe alikubali na tumemalizana nao kwa amani kabisa kwa kuwa Juma Mwambusi amechukuliwa kwa muda mpaka pale Kocha mkuu atakapopatikana kwani hakufukuzwa na baada ya mazungumzo naye alikubali na ikumbukwe kuwa tulichangia gharama za matibabu.


“Kwa kuwa amepona na yeye mwenyewe amekubali kurudi mpaka Alhamisi tumepokea zaidi ya 72 za watu wapya na wengine ni wa zamani na nyingine zinaendelea kuja, “.


Kwenye mechi sita za mwisho za Cedric Kaze katika mzunguko wa pili alishinda mechi moja ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo alishinda bao 1-0, Uwanja wa Mkapa kwa pasi ya Tuisila Kisinda na lilifungwa na Carlos Carinhos.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA WA YANGA AWATULIZA MASHABIKI, AZUNGUMZIA MSIMU WAKE NI ZAIDI YA NABI