Home Simba SC MGOSI: ACHA KAZI IENDELEE

MGOSI: ACHA KAZI IENDELEE

 


LICHA ya kuwa katika majonzi makubwa kutokana na kuondokewa kwa Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli, kikosi cha Simba Queens kimeendelea kujipanga vizuri kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa kufanya mazoezi mara moja kwa siku.

Akizungumzia programu zao za mazoezi Mussa Mgosi amesema: “Kama Watanzania na kwa niaba ya Simba Queens niseme kuwa, tumeghubikwa na majonzi makubwa kwa kuondokewa na Rais John Pombe Magufuli.

“Na licha ya kuwa katika hali hii ya majonzi, bado tunaendelea kumuenzi Rais kwa sera yake kufanya kazi na kujituma kwa kuendelea na mazoezi ambayo kwa sasa tunafanya mara moja kwa siku kulinganisha na mara mbili ambazo tulikuwa tukifanya hapo mwanzo.”

SOMA NA HII  YANGA WAKIZUBAA TU...MWAMNYETO HUYOOO MSIMBAZI...VIGOGO SIMBA KUKUTANA NA WAKALA WAKE LEO..