Home Yanga SC MWAKALEBELA : SIMBA ITAFUNGWA MECHI MBILI ZIJAZO..SISI TUTAKUWA BINGWA VPL

MWAKALEBELA : SIMBA ITAFUNGWA MECHI MBILI ZIJAZO..SISI TUTAKUWA BINGWA VPL


YANGA wanaamini kwamba Simba itapasuka mechi moja au mbili kwenye viporo vyake vya kuelekea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Mbio za ubingwa msimu huu bado zipo wazi kwa timu mbili kutokana na mwenendo wao ulivyo Yanga ambao ndio vinara pamoja na Simba ambao wanashika nafasi ya pili katika msimamo.

Yanga ndio vinara wa ligi katika wamecheza mechi 23, wameshinda 14, wametoka sare nane, wamefungwa moja, wamefunga mabao 36, wamefungwa mabao 14 wamekusanya pointi 50.

Simba wapo katika nafasi ya pili wamecheza mechi, 20 wameshinda 14, wametoka sare nne, wamefungwa mbili, wamefunga mabao 45, wamefungwa sita na pointi ambazo wanazo ni 46.

Kutokana na msimamo ulivyo kama Simba atashinda mechi zake tatu za viporo atakuwa kileleni mwa ligi akimzidi mpinzani wake Yanga pointi tano.

Kutokana na msimamo huo ulivyo Makamo Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameibuka na kusema kuwa hawana wasi wasi wowote na wapinzani wao wakubwa Simba hata kama watashinda mechi zao tatu za viporo.

Mwakalebela ameliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa Simba wakishinda viporo vyao watakuwa kileleni kwa kuwazidi pointi tatu jambo huku wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja wa ligi ambao utakuwa wa mzunguko wa pili na utachezwa mwezi Mei.

“Wala hatuna wasi wasi na Simba kwani hizo hesabu za kuzipunguza pointi tano ambazo wametuzidi wala si ngumu zitakuwa hivi, tunaimani katika michezo yao waliobaki nayo watapoteza miwili au mmoja,” alisema.

“Kama ikitokea wakipoteza mmoja maana yake watakuwa wametuzidi pointi mbili, ambazo tutakuja kuzichukua kibabe tena kifua mbele katika mechi yetu ya marudiano ambayo utakuwa mwishoni mwa ligi na sisi ndio tutakuwa vinara kwa pointi moja dhidi yao.

“Kutokana na hesabu hizo bado Yanga tunaamini mbio za ubingwa msimu huu zipo wazi na tunaendelea kufanya maandalizi ya kutosha katika kikosi chetu ili kwenda kupata matokeo mazuri katika mechi zote ambazo zimebaki na kufikia malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  WAKATI WENZAKE WAKIZIDI 'KUINJOI' YANGA....ISHU YA KIBWANA NA WENZAKE IMEFIKIA HAPA...NABI 'ASUSIWA'...

ISHU YA KOCHA IPO HIVI

Katika hatua nyingine Mwakalebela alisema kuhusu mchakato wa kocha mpya ambaye atakuja kuchukua nafasi ya Mrundi Cedrick Kaze ambaye ameondoka ulikuwa unaendelea ila kifo cha aliyekuwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesimamisha.

“Miongoni mwa makocha ambao wameomba kazi wapo kutoka Tanzania, Afrika, Yugoslavia na nchi mbalimbali za Ulaya ambayo kati ya hao tunaimani tutampata mmoja aliyekuwa bora na kumpa kazi hiyo na atatufikisha katika malengo yetu,” alisema.

“Mambo ni mazuri kwetu wa wapenzi na mashabiki wa Yanga wakae mkao wa kula muda wowote kuanzia sasa tutamtangaza kocha wetu mpya kwani tupo katika hatua za mwisho kukamilisha hili zoezi ambalo lilikuwa likiendesha na watu wenye uweledi mkubwa katika masuala ya kiufundi,” alisema Mwakalebela.

Gazeti la Mwanaspoti linajua kwamba Sebastian Migne ambaye aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Kenya ndiye Kocha Mkuu wa Yanga.