Home Namungo FC NAMUNGO WAIFUATA RAJA CASABLANCA WAKIWA ‘FULL MZUKA’

NAMUNGO WAIFUATA RAJA CASABLANCA WAKIWA ‘FULL MZUKA’


MSAFARA wa watu 32 wa timu ya Namungo umeondoka Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Machi 8, kuelekea nchini Morocco katika mchezo wao wa kwanza wa makundi.

Namungo wawakilishi pekee katika michuano ya Kombe la Shirikisho, inatarajia kushuka dimbani Machi 10 kuwakabili Raja Casablanca katika mchezo wa kwanza wa kundi D.

Katika msafara huo Namungo imeondoka na wachezaji 22 benchi la ufundi sita pamoja na viongozi wanne tayari kwa mtanange huo unaotazamiwa kuwa na ushindani zaidi.

Mwenyekiti wa Namungo Hassan Zidadu amesema kuwa, msafara huo bado haujafika kwa sasa, lakini haujakumbana na kikwazo kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita walipokwenda Angola kuwavaa Agosto.

“Wachezaji wetu wako poa na nimewasiliana nao muda si mrefu wako njiani, nitawatafuta baadae kujua kama wamefika, ila safari ni nzuri wameondoka na ndege ya abiria,”amesema.

Amesema katika mchezo huo Machi 10 wanaimani watafanya vizuri japokuwa wanatambua ushindani na wapinzani wao utakuwa mkubwa kulingana na uwezo wao katika michuano hiyo.

Wapinzani hao wa Namungo, Raja Casablanca ni mabingwa wa taji la mshindano hayo mwaka 2018 lakini pia wamewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu ambazo ni 1989, 1997 na 1999.

Pyramids FC wenyewe msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya pili ya mashindano hayo baada ya kufungwa na RS Berkane katika fainali.

Mafanikio makubwa kwa Nkana FC yalikuwa ni kutinga hatua ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1990 wakati Namungo FC ndio wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Namungo yuko na Raja Casablanca, Pyramids FC, Nkana FC katika kundi lao ambapo anatakiwa kupambana zaidi ili kusonga mbele, lakini kwa hatua hiyo ana uhakika wa kujinyakulia zaidi ya sh mil 600 kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

SOMA NA HII  KISA MAYELE KUTETEMA JANA...KICHUYA AWEKA UNAFKI PEMBENI....AFUNGUKA KAZI ALIYOIFANYA...