Namungo FC

NAMUNGO FC KAMILI GADO KUWAVAA NKANA LEO KWA MKAPA

admin April 4, 2021 3:47 am


 HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana FC ya Zambia na wanahitaji pointi tatu.

Namungo ipo kundi D, imecheza mechi mbili na kupoteza zote, ilianza kupoteza mbele ya Raja Casablanca bao 1-0 ugenini na ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Pyramids, Uwanja wa Mkapa.

Inakutana na Nkana FC ambayo nayo haijakusanya pointi baada ya kupoteza mechi zake zote mbili kwenye makundi jambo ambalo litaongeza ugumu kwenye mchezo huo.

Morocco amesema  kila kitu kipo sawa wanaamini watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa leo.

 “Tumeshindwa kwenye mechi zetu ambazo zmepita tutakuwa nyumbani tutapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Kiujumla wachezaji wapo sawa na morali yao ni kubwa hivyo mashabiki watupe sapoti na dua zao tunazihitaji,” amesema.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI GOMES AMPA MBINU AME KUPENYA KIKOSI CHA KWANZA MBELE YA ONYANGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply