CAF

NKANA FC WAGOMA KUFANYIA MAZOEZI UWANJA WA MKAPA

admin April 4, 2021 1:47 pm


 WAPINZANI wa Klabu ya Namungo leo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Nkana FC wamegoma kufanyia mazoezi ya kupasha misuli ndani ya Uwanja wa Mkapa na badala yake wamefanya nje.

Nkana FC inatarajiwa kumenyana a Namungo FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00.

Timu zote kwenye kundi lao D hakuna ambaye amevuna pointi kwenye mechi mbili ambazo walicheza kwa sababu walipoteza hivyo leo wanaanza upya kusaka pointi.

Wakati walipokuwa kwenye maandalizi ya mchezo huo jana, Kocha Mkuu wa Nkana FC, Kelvin Kaindu alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu.


NKANA PIA WAGOMEA KUINGIA UWANJANI KUMENYANA NA NAMUNGO FC KOMBE LA SHIRIKISHO: NAMUNGO 0-0 NKANA FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply