CAF

NKANA PIA WAGOMEA KUINGIA UWANJANI KUMENYANA NA NAMUNGO FC

admin April 4, 2021 1:47 pm


 KLABU ya Nkana FC ya Zambia imegoma pia kuweza kuingia Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kuanza mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa.


Awali iligoma kufanya mazoezi katika Uwanja wa Mkapa na ilifanyia nje ya uwanja sehemu ya parking ya magari.


Mchezo wa leo ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na timu zote zipo kundi D na kati ya hizo hakuna hata moja ambay imeweza kushinda mchezo hata mmoja kati ya miwili ambayo imecheza.

Sababu ya Nkana kufanya hivyo ni kile ambacho wanadai kuwa kuna hujuma ambazo wamefanyiwa na wapinzani wao.

Pia wamegoma kufanya vipimo vya Corona kwa maelezo kuwa wamepima nchini Zambia hivyo hawawezi kupima kwenye ardhi ya Tanzania.

Namungo wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao ni wa tatu kwenye hatua ya makundi ndani ya Kombe la Shirikisho.

BARAZA ATAMBA KUUWASHA MOTO KAGERA SUGAR NKANA FC WAGOMA KUFANYIA MAZOEZI UWANJA WA MKAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply