Ligi Kuu

KMC YAANZA KUIVUTIA KASI YANGA

admin April 5, 2021 1:47 pm


 KIKOSI cha KMC yenye maskani yake Kinondoni jijini Dar, kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga ambao unatarajiwa kupigwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

KMC imekuwa kwenye kiwango bora msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara ikishinda mechi 10 kati ya 24 walizoshuka uwanjani ikishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi kuu Bara.

 

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Habib Kondo amesema: “Kikosi tayari kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu na Yanga na mechi za Kombe la Shirikisho.


 “Malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote zilizosalia ili tuweze kumaliza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.


“Ushindani kwenye ligi umeongezeka ukizingatia kila timu inapambana kumaliza kwenye nafasi nzuri hivyo ni lazima tufanye maandalizi ya kutosha ili tuweze kufanya vizuri kwenye kila mechi ikiwemo mechi yetu dhidi ya Yanga, “.


KMC inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 35 baada ya kushuka dimbani kwenye mechi 24 wakishinda mechi 10, sare tano na wamepoteza mechi tisa.


Mchezo wa mzunguko wa kwanza KMC ilipokutana na Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba, ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.




BAKARI MWANYETO JEMBE LA KAZI YANGA LICHA YA MAKOSA YANAYOIGHARIMU TIMU HATMA YA RAMOS NDANI YA REAL MADRID YAAMULIWA NA WAZAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply