CAF

SIMON MSUVA APATA KIBURI KISA MABAO YA LIGI YA MABINGWA

admin April 5, 2021 6:47 am

 


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Wydad Casablanca ya Morocco, Mtanzania, Simon Msuva amefichua kuwa ndoto zake msimu huu ni kuhakikisha anakuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msuva mpaka sasa ameshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo na timu yake ipo kundi C.

 

 Msuva amesema kuwa malengo yao katika michuano hiyo ni kuchukua ubingwa pamoja na kuwa mfungaji bora kutokana na kuanza vizuri.


“Kwanza Wydad ni timu kubwa ambayo itanifanya nionekane zaidi na tunashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Afrika lakini pia ubingwa wa Morocco.

 

“Lakini nashukuru nimeweza kuanza vizuri na tayari nimeshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi na sasa matumaini yangu ni kuendelea kupambana ili ikiwezekana niwe mfungaji bora wa michuao hii ambayo itaongeza kitu kwenye wasifu ‘CV’ wangu,” amesema Msuva.

YANGA WAFUNGUKIA UJIO WA MANJI NYOTA WAWILI YANGA WANAUMWA, WAVURUGA MIPANGO YA MWAMBUSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply