Simba SC

TANZANIA KUTOA TIMU NNE KIMATAIFA, MCHORO MZIMA UPO NAMNA HII

admin April 6, 2021 7:47 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuendelea kuwaombea dua wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ili waendelee kufanya vizuri kwa sababu ni faida kwa Tanzania kiujumla.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa msimu ujao Tanzania ikatoa timu nne kwenye mashindano ya kimataifa jambo ambalo ni la kujivunia na linasababishwa na wawakilishi wa Tanzania kwa wakati huu kwenye mashindano ya kimataifa.

Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiwa kundi C na ina pointi 13 baada ya kucheza mechi tano mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili, 9 na leo kikosi kinatarajiwa kukwea pia.

Manara amesema:-“Watanzania watuombee kwa kuwa katika hili faida ni kubwa na kwa namna ambavyo tunakwenda sioni kama kuna nafasi kwa nchi nyingine kutuzidi kweye nafasi ya timu zitakaocheza kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

“Matumaini yetu ni kwamba kutakuwa na timu nne msimu ujao na hii imesababishwa na namba ya pointi ambazo Simba imeipata labda na Namungo pia.

“Simba inakwenda kutupa pointi ambazo mwakani Tanzania kutakuwa na timu nne ambapo mbili Kombe la Shirikisho na mbili Ligi ya Mabingwa,”.



PEP GUARDIOLA ANAMHITAJI HAALAD NDANI YA MANCHESTER CITY TANZANIA PRISONS MGUU SAWA KUENDELEA NA PIRA GWARIDE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply