Simba SC

KIKOSI CHA SIMBA CHAWASILI MISRI

admin April 7, 2021 12:47 pm


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes raia wa Ufaransa leo Aprili 7 kimewasili salama nchini Misri kikitokea Dubai.

Simba ilianza safari ya kuwafuata wapinzani wao Al Ahly jana Aprili 6 kutoka Tanzania na kilipitia Dubai ambapo kilipumzika na leo kilisafiri kuelekea Misri.

Kinatarajiwa kumenyana na Al Ahly Aprili 9, Uwanja wa Taifa wa Cairo kwenye mchezo wa hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly na timu zote zimetinga hatua ya robo fainali.

Simba ni kinara wa kundi A akiwa na pointi 13 huku Al  Ahly akiwa nafasi ya pili na pointi 8.


MRUNDI WA YANGA APEWA PROGRAM MAALUMU TFF YAMJIBU MWAKALEBELA KUHUSU HUKUMU YAKE YA MIAKA MITANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply