LIGI Kuu Tanzania Bara leo Aprili 8 inatarajiwa kuendelea kuchezwa mzunguko wa pili baada ya siku 21 za maombolezo kufuatiwa kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbeya City iliyo nafasi ya 16 na pointi 20 itawakaribisha Kagera Sugar iliyo nafasi ya 13 na pointi 25, Uwanja wa Sokoine.
Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na pointi 27 itawakaribisha Ihefu iliyo nafasi ya 17 na pointi 20, Uwanja wa Majaliwa.