Yanga SC

LAMINE MORO:- WANAYANGA MJE KWA WINGI KESHO UWANJANI

admin April 9, 2021 2:47 pm

 


NAHODHA wa Yanga, Lamine Moro sio mchezaji wa kukata tamaa katika majukumu yake, ameyasema hayo kuelekea mchezo wao dhidi ya KMC utakaopigwa kesho Jumamosi ya Apri 10, 2021 kwamba wapo tayari kwa mapambano.

Moro ameyasema hayo leo Ijumaa, kwamba wamejiandaa vya kutosha wana imani kwamba watanyakua pointi tatu katika mchezo huo.

“Tangu nijiunge na Yanga sijawahi kuona mechi rahisi, kila tunapocheza ushindani unakuwa wa juu, lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu hilo ndilo jambo la msingi kwetu,” amesema na ameongeza kuwa;

“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kutuunga mkono, naamini hatutawaangusha tutapambana kwa kadiri tutakavyoweza kwa ajili ya kuhakikisha timu yetu inaendelea kuwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu,” amesema.

Amesema wameyatumia mapumziko kujiweka sawa na matunda ameyaahidi kuonekana dhidi ya KMC, timu ambayo ina ushindani wa hali ya juu.

SAMATTA ATOA “GUNDU” FENERBAHNCE BARBARA AWAPIGIA “SALUTI” AL AHLY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply