PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC jana alikuwa nyota wa mchezo wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam 2-0 Mtibwa Sugar kwa kutupia mabao yote mawili.
Dakika ya 8 alipachika bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Mudathir Yahya ambaye alichezewa faulo ndani ya 18 na lile la pili alifunga dakika ya 86 na kuifanya timu hiyo kusepa na pointi tatu mazima.
Ushindi huo unaishusha Simba nafasi ya pili mpaka ya tatu kwa kuwa Azam FC imefikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 na Simba ina pointi 46 ikiwa imecheza mechi 20 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 50.
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-0 Azam hivyo jana kisasi kimelipwa. Dube anafikisha jumla ya mabao 10 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara.
STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam