Simba SC

WAWA: YANGA WASIJISAHAU, TUNA JAMBO LETU

admin April 11, 2021 2:47 pm

 


BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ameibuka na kutoa kauli ya vitisho kwa wapinzani wao Yanga  katika Ligi kuu Bara kuwa, wasisahau kwa kujua Simba haina mpango na ubingwa kutokana na ushiriki wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia malengo yao, Wawa amesema kuwa kitendo cha wao kuwa bize na michuano ya kimataifa, isiwe sababu ya wapinzani wao wakiwemo Yanga, kuona urahisi kwa kuweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwani hata wao bado wana malengo na kombe hilo.

“Unajua hii michuano ya  Ligi ya mabingwa Afrika ni migumu sana,  lakini kadiri tunavyopiga hatua ndiyo matarajiao na malengo yetu yanazidi kuwa makubwa.

“Nadhani kuwa bize huku kusiwe sababu ya wengine  kusahau kuwa bado kuna mechi za ligi, kwa sababu licha ya kushiriki ligi ya mabingwa bado tunahitaji kushinda ubingwa wa ndani wa ligi hivyo haiwezi kuwa jambo rahisi,” amesema Wawa.

LWANDAMINA: TUNAITAKA NAFASI YA YANGA HITIMANA ATUMIWA TIKETI KUIMALIZA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply