Simba SC

ONYANGO: TUTAPAMBANA TUSIFUNGWE

admin April 14, 2021 7:47 am


 JOASH Onyango beki wa kati wa Simba amesema kuwa wataendelea kupambana kuzuia kutokufungwa kwenye mechi zote ambazo watacheza.

Leo Aprili 14, Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Imetoka kumalizana na Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Timu hizo mbili zote zimetinga hatua ya robo fainali wakitokea kundi A ambapo kinara ni Simba mwenye pointi 13 na Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 11.

Onyango ambaye kwenye ligi ametupia bao moja amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote na watapambana ili wasifungwe.

“Tumemaliza mashindano ya kimataifa hatua ya kwanza na tunaamini kuna hatua nyingine ambayo inakuja tupo tayari kwa ajili ya robo fainali na tutapambana ili tupate matokeo mazuri kwa kulinda lango ili tusifungwe.

“Kwenye ligi pia tunazidi kupambana ili kupata matokeo mazuri, kila kitu kinawezekana na tutazidi kushindana kila wakati,” .

YANGA WATAJA SABABU YA NCHIMBI KUCHUKUA MIKOBA YA MUKOKO NADO ATAJA SABABU ZA KUSAINI DILI JIPYA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply