UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweomba mashabiki na wanachama wa Yanga kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi pale wanapobaini kuna tatizo.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tabia ya mashabiki kusema matatizo yao mitandaoni kila kitu hayaleti picha nzuri.
Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC mashabiki wa Yanga walikuwa wakilalamika kwa kusema kuwa mwendo ambao wanakwenda nao hauwapi fuaraha zaidi ya stress.
Bumbuli amesema:-“Wanachama na mashabiki waache tabia ya kutaka umaarufu kwa kuzungumza, kama wameona tatizo baada ya mechi waje klabuni kusema au watupigie simu maana wanazo namba zetu.
” Ukisema unawapa faida vyombo vya habari halafu wachezaji wanawachanganya safari ya ubingwa inahitaji uvumilivu,”.
Kwenye msimamo wa ligi Yanga ina pointi 51 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 24.