Ligi Kuu

JUMA KASEJA: KMC INA KIKOSI BORA, BADO TUNAPAMBANA

admin April 15, 2021 8:47 am

 


JUMA Kaseja, nahodha wa kikosi cha KMC amesema kuwa wachezaji wote wa kikosi cha KMC ni bora jambo ambalo linampa nafasi kocha kuchagua aina ya wachezaji anaotaka waanze kikosi cha kwanza.

Mkongwe huyo kwenye eneo la milingoti mitatu aliwahi kucheza kwa mafanikio ndani ya kikosi cha Smba ambapo huko pia alikuwa ni nahodha, pia amecheza Yanga, Kagera Sugar na Mbeya City.

 Kaseja amesema kuwa jukumu la kocha ni kujua aina gani ya wachezaji ambao anahitaji waanze kwa sababu wote wapo vizuri na wanashirikiana.

“Timu ipo vizuri na hiyo inampa chaguo  mwalimu kujua ni nani ataanza kikosi cha kwanza. Wachezaji tukiwa kambini tunashirikiana na kutimiza majukumu kwa wakati.

“Tukipata matokeo tunafurahi na pale ambapo tunashindwa ni kazi ya kufanyia kazi makosa ambayo tunayafanya ila kikubwa ni kwamba tupo imara na tayari kwa ushindani na tunaendelea kupambana,” amesema.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, KMC ipo nafasi ya 6 imekusanya pointi 36 baada ya kucheza mechi 25.

GOMES WA SIMBA AWACHAMBUA WAPINZANI WAO KIMATAIFA MTAMBO WA MABAO YANGA RUKSA KUWAVAA BIASHARA UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply